Mnada wa nyumba ya mfanyabiashara, Lugumi uliomalizika Leo mchana Novemba 24 Mbweni JKT umesitishwa baada ya wanunuzi kushindwa kufikia bei elekezi, mnunuzi wa juu amefikia Sh.510 milioni.

Katika mnada huo unaoendeshwa na kampuni ya Yono, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Scholastika Kevela amesema wateja waliojitokeza wamefikia Sh510 milioni ambayo iko chini ya mategemeo.

“Tunahamia nyumba ya Upanga, kama atapatikana mteja leo tunaweza kurudi na tukamuuzia na masharti ni yaleyale kwamba lazima mteja akifika bei alipe hapa hapa asilimia 25 na asilimia 75 ndani ya siku 14,” amesema Kevela

Nyumba hii imeshindwa kununuliwa kwa mara ya tatu baada Septemba 7 kujitokeza kama leo na Novemba 9 ambao unadaiwa ulivurugwa na ‘Bilionea’ Dk Louis Shika.

Tofauti na ulivyokuwa Novemba 9, leo kila aliyefika katika mnada huo alitakiwa kujiandikisha ikiwamo waandishi wa habari huku ulinzi ukiwa umeimarishwa zaidi .

Kingue aongozewa mwaka mmoja Azam FC
Ndalichako ashikilia kidete ujenzi nyumba za walimu