Mshambuliaji kutoka nchini Misri ba Klabu ya Liverpool, Mohamed Salah, amesisitiza hakuna kisingizio cha wao kukosa kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao 2023/24.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekiri timu hiyo imeshindwa na imewaangusha mashabiki msimu huu kwa kutomaliza katika nafasi nne za juu.

Ushindi wa Manchester United wa mabao 4-1 dhidi ya Chelsea juzi Alhamis (Mei 25) ulimaanisha Liverpool haiwezi kumaliza katika nne bora na rasmi hawatacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kikosi cha Jurgen Klopp kimefanya vibaya msimu mzima na sasa kitashiriki kwenye Ligi ya Europa.

Na hilo limemfanya Salah kutopendezwa nalo na amesema: “Nimevunjika moyo kabisa. Hakuna kujitetea katika hili.

“Tulikuwa na kila kitu tulichohitaji ili kufikia Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.”

Katika msimu wa kusikitisha, Salah bado amefunga mabao 30 na amebakiza moja pekee kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kufunga mabao 20 na asisti 10 ndani ya misimu mitatu, ambayo ingevuka rekodi aliyowekwa na Thierry Henry.

Ana upungufu wa kufikisha mabao 20 katika msimu mmoja kwa mara ya tano ndani ya miaka sita ndani ya Liverpool alifunga mabao 19 kwa mwaka mwingine na kama atafanikiwa kufunga dhidi ya Southampton Jumapili, atakuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool tangu Roger Hunt msimu wa 1965-66 kufunga mabao 20 ya ligi kwa misimu mitatu mfululizo.

Pokies slots on phone
Title: Meridianbet Yazindua Duka Jipya Ubungo-Kibangu