Moto umelipuka katika wodi moja ya hospitali ya Groote Schuur jijini Cape Town nchini Afrika kusini na kusababisha kifo cha mtu mmoja mwenye umri wa miaka 63 aliyekuwa amelazwa ndani ya wodi hiyo.

Msemaji wa hospitali hiyo, Alaric Jacobs amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili majira ya saa nne usiku ambapo wafanyakazi walipigia simu kikosi cha uokoaji kilichowasili muda mfupi baadaye.

“Wafanyakazi wetu walipiga simu haraka kwa kikosi cha uokoaji na kuwaondoa wagonjwa wote ndani ya wodi hiyo. Kikosi cha uokoaji kilifanikiwa kuuzima moto huo kabla haujaathiri wodi nyingine.

Ameongeza kuwa hakuna mgonjwa mwingine aliyepata majeraha kutokana na moto huo na akatoa pole kwa familia ya mgonjwa aliyepoteza maisha.

Jacobs ameeleza kuwa idara ya afya inafanya kazi kwa karibu na jeshi la polisi kuhakikisha kuwa wanabaini chanzo cha moto huo.

Chuo cha IFM mabingwa ligi ya vyuo
Luoga aanza kazi rasmi na mikakati mizito