Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ametoa sababu kwa nini aliamua kuitoa zawadi medali yake ya fedha kwa shabiki wa Arsenal ambaye alihudhuria mchezo wa kuwania ngao ya jamii kwenye uwanja wa Wembely huko jijini London hapo jana.

Mourinho, ambaye hakupendezwa na kitendo cha kikosi chake kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri katika mpambano huo ambao ulikua unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kote, amesema aliamua kufanya hivyo kwa kuona hakuna sababu kwake kukaa na medali ya mshindi wa pili.

Mourionho

Amesema aliamua kuitoa zawadi kwa shabiki wa Arsenal ili iwe kumbu kumbu kwake, na hajutii kitendo hicho ambacho anakichukuli kama cha kishujaa.

Mourinho, alionekana akimrushia kasha lililokua na medali yake, mtoto aliyekua amekaa upande wa mashabiki wa Arsenal dakika chache baada ya kushuka kutoka jukwaa kuu alipokua amekwenda kukabidhiwa zawadi hiyo sambamba na wachezaji wa Chelsea.

Soldado Kurejeshwa Nchini Hispania
Rais Nkurunzinza Atoa Onyo Baada Ya Mauaji Ya Jenerali Wa Jeshi Lake