Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza ametoa onyo kwa raia wa nchi hiyo kuachana tabia ya kulipa visasi  kwa kuwa ni hatari kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Onyo hilo la Nkurunzinza linakuja ikiwa ni siku chache tangu watu waliovalia mavazi ya kijeshi kumuua generali wa ngazi ya juu wa jeshi la Burundi, Adolphe Nshimirimana.

Mauaji hayo yalitokea siku chache baada ya Nkurunzinza kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa urais uliolalamikiwa na wapinzani wake kuwa alikiuka matakwa ya katiba na kugombea muhula wa tatu.

Rais huyo wa Burundi pia aliamuru kitengo cha usalama wa taifa na ujasusi kufanya uchunguzi wa haraka kubaini chanzo na watekelezaji wa mauaji hayo.

Gen. Adolphe Nshimirimana

Gen. Adolphe Nshimirimana

“Burundi imempoteza mtumishi mkubwa, jenerali Adolphe Nshimirimana alikuwa akifanya kazi kwa bidii. Natoa wito kwa idara ya usalama kuanzisha uchunguzi ndani ya wiki moja ili wahalifu watambuliwe na kushtakiwa. Nawataka raia wote wa Burundi kuwa watulivu na kuungana,” alisema rais Nkurunzinza.

Mourinho Aeleza Sababu Za Kuigawa Medali Yake
Jeshi La Nigeria Lawakalia Kooni Boko Haram, Kiongozi Wao Atoweka