Wanajiolojia wamethibitisha uwepo wa nyufa kubwa inayolitishia bara la Afrika kugawanywa na maji na kutoka vipande viwili kutokana na ufa wenye urefu wa maili 35 kuonekana katika jangwa la Ethiopia lililopo eneo la Far na kutoa uwezekano wa kutokea kwa bahari mpya.
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la Barua za Utafiti wa Geophysical, umeeleza kuwa data ya tetemeko ya uundaji wa ufa inaendeshwa na michakato sawa na ile iliyo chini ya bahari na kwamba sahani za kiinuko za Afrika na Uarabuni zinagongana jangwani na zimekuwa zikitengana polepole kwa takriban miaka milioni 30.
Utafiti huo umeendelea kueleza kuwa, mwendo huo pia umegawanyika katika Bahari Nyekundu, na kwamba hali hhiyo hutokea kwa kiwango cha sehemu ya inchi kwa mwaka huku watu wengi wakishitushwa na hali hiyo ya taarifa za Bahari mpya.
Kwa mujibu wa Dkt. Edwin Dindi wa Idara ya Jiolojia katika Kitivo cha Sayansi na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Nairobi, amesema hali hiyo inaweza kutokea kwenye bahari kando ya mkono wa mashariki wa Bonde la Ufa la Afrika.
“Mkono wa Mashariki wa Bonde la Ufa unafanya kazi ipasavyo, hii inaonekana katika mitetemeko mingi inayotokea karibu nayo hata hivyo, itachukua muda mrefu pengine mamilioni ya miaka kwa hali kama hiyo kutokea, na mfumo huo una urefu wa kilomita 6,400 na wastani wa kati ya kilomita 48 hadi 64 kwa upana.
Amesema, mabadiliko hayo yametokea kwenye maeneo yenye kasoro, huku mengine yakianguka chini ya jingine na yakigongana na tengana kwenye sahani tofauti na kwamba hali kama hiyo ndiyo ilisababisha kuundwa kwa mabara mbalimbali tunayoyafahamu hii leo, likiwemo la Afrika, Amerika ya Kusini, Amerika Kaskazini, Ulaya, Asia, na Australia.
Kwa mujibu wa Dindi, amesema mwendo unaoendelea ndani ya ukoko wa bara hilo pia umesababisha kuundwa kwa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, ambalo linaendelea kuwa hai na kupanuka na linaweza pia kuunda bahari mpya barani Afrika.
“Lakini hili halitatokea mara moja, ni jambo litakalotokea mamilioni ya miaka ijayo,” anasema Dindi na kuongeza, “kumbuka imechukua zaidi ya miaka milioni 30 kwa unene kuzunguka bonde la ufa kupungua kutoka kilomita 40 hadi kilomita 35, ikimaanisha kwamba itachukua miaka mingi zaidi kumaliza kilomita 5 nyingine.”
Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, pia linajulikana kama Bonde la Ufa la Afro-Arabian, ni mojawapo ya mipasuko mingi kwenye uso wa Dunia, inayoenea kutoka mto Yordani uliopo kusini magharibi mwa Asia, kuelekea kusini kupitia Afrika mashariki hadi nchini Msumbiji.