Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC), Meja Jenerali Michael Mhona amewaongoza wanafunzi wa chuo chake kufanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Polisi Jijini Dodoma, hii leo Februari 21, 2023.

Akiwa katika makao hayo makuu ya Polisi, Meja Jenerali Michael Mhona alikabidhi Kalenda na Jarida la Polisi na Kamishna wa Intelejensia ya Jinai, CP Charles Mkumbo ambaye ni mmoja wa Viongozi waliwahi kupitia katika chuo hicho.

Kamishna wa Intelejensia ya Jinai, CP Charles Mkumbo akimkabidhi Kalenda na Jarida la Polisi Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC), Meja Jenerali Michael Mhona Makao Makuu ya Polisi Jijini Dodoma hii leo Februari 21, 2023.
Kamishna wa Intelejensia ya Jinai CP Charles Mkumbo akizungumza na Uongozi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC), Makao Makuu ya Polisi Jijini Dodoma hii leo Februari 21, 2023.
Kamishna wa Intelejensia ya Jinai CP Charles Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao Makuu ya Polisi Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao Makuu ya Polisi Jijini Dododma

Waziri kundo ataka uhabarishaji shughuli za kimaendeleo
Rais Samia akutana na Sheikh Shakhboot wa UAE