Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewahakikishia wananchi usalama wa treni ya umeme endapo itatokea changamoto ya umeme mabehewa yatakuwa na uwezo wa kukaa na umeme kwa muda wa saa moja mpaka mawili.
Akizungumza kwenye kikao cha vijana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, katika viwanja vya Nyamagana mkoani Mwanza, Waziri Kalemani amewataka vijana wa kanda ya ziwa na maeneo mengine kujiandaa kutumia fursa ya treni hiyo ya umeme kwa kupeleka bidhaa na kufanya biashara kwa urahisi kutoka Mwanza kwenda Singida, Dodoma mpaka Dar es Salaam.
Aidha, Waziri Kalemani amesema kuwa kupitia mradi huo wafanyabiashara watafaidika na itawarahisishia kusafirisha bidhaa zao.
Halikadhalika Waziri Kalemani amesema kituo cha kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro kimekamilika na hata mabehewa hayo yakija reli iko tayari kutumika, aidha wanaendelea na ujenzi wa reli hiyo mpaka Mwanza.
Sambamba na hayo yote, Waziri Kalemani ameelezea mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ambapo mwezi Julai wanaanza kuchukua vijana wa ajira kwa ajili ya mradi huo.