Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwasili mkoani humo leo Juni 13, kwa ziara ya siku tatu.

Amesema katika ziara hiyo, Rais atazindua miradi mitatu ya kimkakati ambayo ni Kiwanda cha kusafisha dhahabu, Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Kanda ya Ziwa na Mradi mkubwa wa Maji Wilayani Misungwi.

Aidha Rais ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Reli ya kisasa ya kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Fela Isaka na kukagua ujenzi wa mradi wa daraja la John Magufuli.

“Rais Samia atahitimisha ziara hiyo kwa kuzungumza na vijana wa Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya vijana wote Nchini katika Uwanja wa Mpira wa Nyamagana,” amesems RC Gabriel

Kula samaki uishi muda mrefu
Burundi: Waziri akataza adhana isitolewe kwa sauti kubwa, Sheikh amkosoa wenzake wamgeuka