Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon ambao ni mtandao wa biashara, amerejea katika nafasi yake ya kuwa tajiri namba moja duniani.

Hii ni kwa mujibu wa orodha mpya iliyotolewa na Jarida la Forbes, ambapo hisa za kampuni yake ya Amazon zimepanda kwa asilimia 2 kuliko kawaida na kuingiza Dola za Kimarekani bilioni 3.5 kwa siku moja.

Hivyo kwa sasa Bezos ana utajiri wa Dola za Kimarekani bilioni 193.5 ambapo awali alikuwa na Dola za Kimarekani bilioni 186.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Jarida la Forbes kupitia orodha yake juu ya watu matajiri zaidi duniani, lilishtua ulimwengu kwani Mkuu wa Kampuni ya LVMH, Bernard Arnault alimshusha  Bezos na kushika namba moja kwenye orodha hiyo akiwa na utajiri wa Dola za Kimarekani bilioni 186.3 na Bezos alikuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani bilioni 186.

Aliyerekodi tukio la kuuawa George Floyd apewa tuzo
Mtangazaji Fredwaa afariki dunia, Kamanda aeleza chanzo cha kifo chake