Bodi ya tuzo za Pulitzer imempa tuzo ya heshima ya “Pulitzer Prize” na dola za kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh Milioni 34 za kitanzania), Darnella Frazier, msichana aliyerekodi video iliyoonesha tukio la mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd Mwezi Mei Mwaka jana.

Darnella_alikuwa akitembea tu binamu yake mdogo kwenda dukani mnamo Mei 25, 2020, ndipo alipoona mapambano kati ya mtu mweusi na afisa wa polisi Mzungu akarekodi kwa simu yake, tukio hilo kwa muda wa wa dakika 9.

Video hiyo ilitumika kama moja ya ushahidi katika kesi dhidi ya Afisa wa polisi, Derek Chauvin na video yake ilipingana sana na taarifa ya polisi ambayo ilisema kwamba maafisa waligundua Floyd alikuwa na shida ya kiafya baada ya kumfunga pingu na kwamba alipelekwa hospitalini kupitia gari la wagonjwa na ndipo alifariki.

Kifo cha Floyd kilisababisha maandamano makubwa ndani na nje ya Marekani, yaliyolaani matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi dhidi ya raia pamoja na ubaguzi wa rangi.

Tuzo hiyo ya heshima ya pulitzerprizes hutolewa kwa watu waliofanya vitu vikubwa na vizuri kwenye jamii.

Burundi: Waziri akataza adhana isitolewe kwa sauti kubwa, Sheikh amkosoa wenzake wamgeuka
Mmiliki wa Amazon arudi tena kileleni kwa utajiri