Pambano la kisiasa kati ya mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema bado halijakamalizika kama wengi walivyodhani baada ya Mbatia kutangazwa mshindi na kung’oa Mrema kwenye kiti cha ubunge wa jimbo la Vunjo kupitia uchaguzi uliofanyika October 25 mwaka huu.

Mrema ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kabla hajang’olewa na Mbatia na kuhamia TLP, amesema kuwa amepanga kwenda mahakamani kufungua kesi ya kupinga matokeo hayo kwa kuwa anaamini alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo lakini aliibiwa kura.

“Kwa jinsi ninavyowafahamu wananchi wangu wa jimbo la Vunjo walivyo na imani na mimi katika kipindi nilichowaongoza, naamini nilishinda kwa kishindo. Lakini kutokana na wizi wa kura alioufanya Mbatia, kwa kweli ni lazima nimpeleke mahakamani,” alisema Mrema katika sherehe iliyoandaliwa kwa ajili ya vyama vya siasa kumuaga Rais Jakaya Kikwete.

Hatua hiyo ya Mrema iliungwa mkono na aliyekuwa mgombea urais wa TLP, Maxmillian Lyimo.

Wenje Aibukia Namibia, Ajipanga Kumvaa Kivingine aliyemshinda Ubunge
Waangalizi wa Ndani Wakosoa Muundo Wa Tume, Waimulika Zanzibar