Waangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu (TEMCO), wametoa tathmini yao kuhusu mwenendo wa uchaguzi na kuukosoa muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa uhusiano wake na rais.

Akitoa mapendekezo yao, mwenyekiti mwenza wa TEMCO, Dkt. Benson Bana amesema kuwa changamoto kubwa ipo katika muundo wa Tume kwani mwenyekiti na mkurugenzi huteuliwa na Rais wa nchi ambapo kuna wakati rais huyo aliyewateua hugeuka kuwa mgombea anaetetea nafasi yake kwa muhula wa pili. Hivyo, mgongano wa maslahi unaweza kupelekea kutokuwepo na maamuzi huru.

Aidha, Dkt. Bana alieleza kuwa kuna ulazima wa kufanya mabadiliko ya sheria na kuruhusu wagombea binafsi wa nafasi mbalimbali ili kuwapa nafasi watanzania wengi zaidi wenye vigezo kupata haki ya kuwania nafasi za uongozi nchini bila kutegemea vyama vya siasa.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo mwenza wa TEMCO alitoa wito kwa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufikiria upya uamuzi wa kufuta uchauguzi wa Zanzibar ambao ameeleza kuwa ulionekana kufanyika kwa amani na utulivu ili haki iweze kutendeka.

Waangalizi mbalimbali kutoka nje ya nchi wakiwemo waangalizi kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya, Common Wealth na Umoja wa Ulaya walieleza kuridhishwa na jinsi ambavyo uchaguzi uliendeshwa nchini licha kuwepo changamoto mbalimbali walizozibaini. Waangalizi hao wa nje pia walipendekeza muundo wa Tume huru ya Uchaguzi.

 

Mrema Amkaba Tena Mbatia
Beyonce, Tailor Swift wagombea ‘Umaarufu’ kwenye mitandao wa Kijamii