Tailor Swift ambaye hivi karibuni amevunja rekodi ya kuwa na wafuasi wengi zaidi kwenye Instagram amepangwa kuwania tuzo ya umaarufu wa mitandao ya kijamii (Social Media Celebrity) kupitia Tuzo maarufu za Watu (People’s Choice Awards 2016), huku akipambana na Beyonce na Britney Spears.

Familia ya Kim Kardashian imejikuta nje ya kipengele hicho licha ya kuwa na ushawishi na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Katika kipengele hicho, mbali na mastaa hao watatu pia wametajwa Anna Kendrick na Dwayne ‘The Rock’ Johnson.

Akiitoa kimasomaso familia ya The Kardashians, Kylie Jenner pekee ndiye aliyetajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha ‘The Dailymail.com Seriously Popular Award, akichuana na Bella Thorne, Cara Delvingne, Maddie Ziegler na Ruby Rose.

Washindi wa vipengele vyote vya tuzo hizo vinavyojumuisha muziki, filamu na TV watatangazwa wakati wa kilele cha tuzo zilizopangwa kufanyika January 6 mwakani Los Angeles, Marekani, Microsoft Theater.

Mashabiki wanaweza kuanza kuwapigia kura wasanii wanaowakubali zaidi katika vipengele vilivyotajwa kwenye tuzo hizo kupitia www.peopleschoice.com na kupitia ukurasa wao wa facebook, ‘Peoples Choice’.

 

 

Waangalizi wa Ndani Wakosoa Muundo Wa Tume, Waimulika Zanzibar
Nani Anafuata Kupanda Kizimbani Baada Ya Yericco Nyerere?