Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza kupitia Chadema, Ezekiel Wenje aliyeshindwa kwenye uchaguzi mkuu na Stanslaus Mabula wa CCM ameibukia Namibia na kueleza kuwa hajakata tamaa dhidi ya matokeo anayoamini yalimnyang’anya ushindi kwa nguvu.

Wenje alidai kuwa yuko Windhoek Namibia ambapo anashiriki katika mdahalo maalum wa kisiasa uliopewa jina la ‘New Windhoek Dialogue’. Alisema punde atakaporejea kutoka huko atafungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

“Nitarudi siku yoyote kuendelea na mambo yangu ya siasa kama nilivyotangulia kusema kwamba nakwenda mahakamani kupinga ushindi nilioporwa kwa nguvu na kumpa mtu aliyeshindwa,” alisema Wenje.

Katika hatua nyingine, Wenje alieleza kushitushwa na taarifa zilizoenezwa mitandaoni kuwa amefariki baada ya kupigwa risasi hivi karibuni.

Mwanasiasa hiyo aliwataka ndugu jamaa na marafiki kupuuzia taarifa hizo na vyombo vya dola pamoja na TCRA kufanya kazi yake na kumchukulia hatua stahiki mtu aliyesambaza taarifa hizo za upotoshaji.

 

Faidha Kuyaanika Maisha yake na Sugu
Mrema Amkaba Tena Mbatia