Mrembo Faidha Ali ambaye ni mzazi mwenza wa mbunge wa mteule wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi amepanga kuyaweka wazi maisha yake na Sugu kwa jinsi walivyomlea mtoto wao Sasha, kupitia filamu.

Faidha Na Sugu

Faidha amesema kuwa ameuamua kufanya filamu ya maisha ya kweli kuhusu jinsi alivyomlea mtoto wake ‘Sasha’ ili jamii ifahamu alivyokuwa bora katika malezi ya mwanaye tofauti na wengi wanavyoamini hasa kutokana na muonekano wake wa mavazi.

Amesema kuwa filamu hiyo ameipa jina la ‘Baby Mama Drama’ na itamhusisha Sasha, huku uhusika wa baba Sasha (Sugu) ukichezwa na Gabo.

“Nataka kuonesha jinsi nilivyopitia katika maisha yangu tangu nilipompata mtoto Sasha,” alisema Faidha.

Mahakama iliamuru Sugu amchukue mwanae Sasha kutoka kwa mama yake huyo baada ya kufungua kesi akimlalamikia kwa kushindwa kumpa malezi bora mwanaye na kutokuwa mfano mzuri kwa jamii kutokana na mwenendo wake hasa mavazi yasizingatia maadili ya kitanzania.

Faidha na Mwanae Sasha

Uamuzi huo wa mahakama ulipingwa vikali na Faidha aliyedai kuwa ameonewa na kwamba mavazi yake sio kigezo cha kupima jinsi anavyomlea mwanaye.

Hata hivyo, Sugu aliweka wazi Bungeni (bunge lililopita) kuwa hatamchukua mwanaye huyo hadi suala hilo litakapojadiliwa na kutatuliwa katika ngazi ya familia.

 

Nguvu Ya Lowassa Yatajwa Kuamua Spika Mpya
Wenje Aibukia Namibia, Ajipanga Kumvaa Kivingine aliyemshinda Ubunge