Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustine Mrema amewataka wananchi kumrudia Mwenyezi Mungu ili kuweza kuondokana na majanga ambayo yanazidi kujitokeza kila kukicha hapa nchini.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati wa Ibaada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Sinza Jijini Dar es salaam, amesema matukio yanayoendelea kutokea nchini hayakubaliki hata kidogo kwani Tanzania haina historia ya kufanya maovu kama hayo.

Aidha, katika hatua nyingine Mrema ametimiza ahadi yake ya kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za Kanisa Katoliki Sinza.

Mrema amewaasa wananchi wote kuheshimu utawala uliopo na kufichua watu wanaofanya maovu katika jamii ili waweze kuepukana na majanga ambayo yanaendelea kutokea hasa ya ujambazi, mauaji na utekaji unavyoendelea hapa nchini.

“Wananchi tushikamane tuilinde amani ya nchi yetu, tuwafichue hawa waovu wanaotaka kutuvuruga, Rais wetu anafanya kazi kubwa sana hivyo tumuunge mkono kwa kufichua waovu,”amesema Mrema.

Hata hivyo, Mrema amemshukuru, Kadinali Pengo kwa kuzidi kumuombea na kumpatia ushauri mbalimbali ambao unamuwezesha kufanya shughuli za maendeleo ya nchi.

CUF yatoa siku 14 kwa Jeshi la Polisi kuruhu usafi ufanyike Ofisini kwake Buguruni
Trump awashambulia wanahabari akiadhimisha siku 100