Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema anatarajiwa kuzikwa Agosti 25 nyumbani alikozaliwa katika kijiji cha Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Mtoto wa Marehemu, Michael Mrema, amesema Ibada ya kumuaga marehemu itafanyika siku ya Jumatano Agosti 24, katika kanisa Katoliki Parokia ya Salasala, jijini Dar es Salaam kuanzia Saa 7 mchana na baada ya Misa safari ya kuelekea Moshi itaanza.

Mrema alifariki dunia Jumapili Agosti 21, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam baada ya kuugua na kulazwa katika hospitali hiyo.

Wakati maandalizi ya maziko yakiendelea, Mjane wake, Doreen Kimbi ametoa shukrani kwa Watanzania na Serikali kwa kushirikiana na familia hiyo katika kuomboleza kufo cha mwanasiasa huyo.


Sensa: Utulivu watawala zoezi likiendelea
Madaktari waanza uchunguzi mshukiwa wa Ebola