Mwanamitindo na video vixen aliyewahi kutamba kupitia video za wasanii kadhaa wa mziki wa bongo hatimaye ameachiwa huru kutoka gerezani Macao huko nchini China alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka kadhaa tangu alipohukumiwa mnamo mwaka 2014 baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, hasa kuingiza dawa hizo huko Macao nchini China Disemba 2013.

Mapema usiku wa kuamkia leo Nov 16, 2021. kupitia ukurasa wake mpya wa mtandao wa Instagram Jackie amethibitisha kurudi kwake kwenye matumizi ya mtandao wa Instagram akiitambulisha akaunti yake mpya iitwayo (@ms.jackiecliff).

Jackie alikamatwa akiwa na Kilogram 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroine zikiwa mwilini kwake,  Dawa zilizotajwa kuwa na thamani ya zaidi ya Usd 100k za Kimarekani kwa kipindi hicho.

Mrembo huyo ametumikia kifungo hicho kwa kipindi cha takribani miaka nane Gerezani.

Kocha Pablo aomba muda Simba SC
Halmashauri zahimizwa kuzingatia mpango wa matumizi Bora ya ardhi