Mkuu wa wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, amewaasa madereva kuzingatia sheria za barabarani ambapo amesema hata ajali iliyotokea hii leo na kupelekea vifo vya watu 5, chanzo chake ni uzembe wa dereva.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 5, 2020, amesema mpaka sasa dereva hajulikani alipo kwani mara baada ya ajali hiyo alitoweka kusikojulikana.

“Niwape pole familia ambazo wamepoteza wapendwa wao, ambapo mpaka sasa hivi wamefariki 5 na majeruhi 10, inaonekana ni uzembe wa madereva maana wakati wanatoka Buza abiria walikuwa wanamuambia apunguze mwendo na alipofika kwenye mataa taa nyekundu ilikua imewaka, abiria wakamkumbusha lakini akawaambiwa wasimfundishe kazi”, amesema DC Gondwe.

“Dereva yeye kakimbia na serikali ina mkono mrefu tutamfikia, nitoe wito kwa madereva wa dalaladala wamebeba uhai wa watu, mali zinatafutwa, uhai wa mtu ukipotea hauwezi kurejea kwa hiyo wafuate sheria ili kuokoa maisha”. Amesema DC Gondwe.

Ajali hiyo iliyohusisha daladala na lori imetokea leo Oktoba 5, 2020, katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es Salaam, majira ya saa 10:00 alfajiri.

Kesi ya kigogo wa MSD yapigwa kalenda
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 5, 2020