Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania imeleezwa upelelezi wa kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki, Byekwaso Tabura, bado unaendelea

Akieleza hayo yameelezwa leo Oktoba 5, 2020 mbele Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate na upande wa mashiaka wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutwaja ambapo Wakili wa serikali Benson Mwaitenda, amedai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na baada ya Hakimu Kabate kumaliza kusikiliza hoja hiyo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19 mwaka huu.

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili washtakiwa ni kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 June, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa waliongoza genge la uhalifu.

Shtaka la pili ni kuisababishia hasara MSD, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Julai mosi, 2016 na tarehe 30 June, 2019, katika eneo la MSD lililopo Keko, washtakiwa waliisababishia MSD hasara ya shilingi bilioni 3.8.

Pia, Bwanakunu, anadaiwa kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 Juni, 2019 katika Ofisi za MSD zilizopo Keko, kwa makusudi alikiuka sheria ya umma kwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwaongezea nyongeza ya mishahara na posho wafanyakazi wa MSD, bila kibali cha Katibu Mkuu Utumishi na hivyo kuisababishia hasara mamlaka hiyo kiasi cha shilingi bilioni 3.

Shtaka la nne ni kuisababishia hasara ya shilingi 85 milioni mamlaka, shtaka linalowakabili washtakiwa wote, huku katika shtaka lingine wakituhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.6.

Wasichana kunyanyasika mtandaoni
''Msinifundishe kazi''- Dereva ajali ya Temeke