Mtendaji wa Kijiji cha Malamba kata ya Ruiwa, Nelson Lupakisyo, amefutwa kazi na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwenye kikao cha mwaka.

Baraza hilo limefikia uamuzi huo baada ya Mtendaji, Lupakisyo kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili na Mahakama.

kikao hicho ambacho ni cha mwisho cha baraza hilo, ambalo limedumu katika kipindi cha miaka mitano, kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbarali, Brown Mwakibete ,

Aidha Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mwajabu Abdalah Nyamkomora ametoa tahadhari kwa Maafisa watendaji kwenyesuala la usimamizi wa miradi.

CCM yatangaza siku 15 za mchuano kumpata mgombea urais 2020
RAIS NKURUNZIZA: Kocha aliyehukumiwa kifo akaangukia URAIS, vita na mapenzi - Makala