Kijana Honest Mulokozi Juventusi (15) aliyekuwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rubya Seminari ya Muleba Mkoani Kagera, amefariki Dunia  baada ya kugongwa na Gari la Mizigo akitokea kutazama matokeo yake ya Kidato cha Pili.

Ajali hiyo iliyotokea mnamo Tarehe 09 Januari 2020, eneo la Optima Bunazi Wilayani Missenyi ikihusisha  Gari aina ya Roli (Fuso) yenye namba za usajili T612 BGJ mali ya Kanyomoza, likiendeshwa na Dereva aliyefahamika kwa Jina la Felix France Bayenda (27).]

Imeelezwa kuwa gali hilo liligonga Pikipiki aina Bajaji Boxer  yenye namba za usajili T 670 BNF Mali ya Kachecheba Brighton  iliyokuwa ikiendeshwa na Marehemu Honest Mulokozi, wakati akitokea kutazama matokeo yake pamoja na matokeo ya Dada yake.

Shuhuda Wa ajali hiyo wanasema marehemu Honest akiwa anaendesha pikipiki hiyo alijaribu kuwakwepa wanafunzi waliokuwa wakitembea upande wake, hivyo akahamia katikati ya barabara na Kwa bahati mbaya tayari Roli hilo likitokea Nyuma yake licha ya Dereva kujaribu kumkwepa, sehemu ya nyuma ya gari hilo ilimgonga na kumsababishia Kifo.

Tayari Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo, na Mwili wa Marehemu umehifadhiwa Chumba cha Maiti katika Hospitali ya Bunazi taratibu za mazishi zikiendelea.

 

Video: Umeya wa jiji Dar sasa kizungumkuti, Chadema waanza mwaka vibaya
Iran yakiri kutungua ndege ya abiria ya Ukraine, Rais atoa tamko

Comments

comments