Rais Robert Mugabe ambaye ndiye rais aliyekula chumvi nyingi zaidi duniani, ameongeza chumvi nyingine Jana kimyakimya.

Mzee Mugabe ametimiza umri wa miaka 92 jana (Februari 21) na kufanya hafla ya kimyakimya tofauti na ilivyokuwa miaka iliyopita ambapo siku yake ya kuzaliwa ilisherehekewa katika uwanja mkubwa wa mpira nchini humo.

Taarifa za awali zilizoripotiwa na Shirika la Habari la SABC zilieleza kuwa Rais huyo alikuwa anatarajia kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa kufanya sherehe kubwa wiki ijayo ambayo ingegharimu kiasi kikubwa cha fedha.

Watu wengi walimtakia heri ya siku ya kuzaliwa kupitia mitandao ya kijamii, huku baadhi ya nukuu zinazoaminika kuwa zake zikisambazwa na watumiaji hao.

Rais Mugabe alizaliwa Februari 21 mwaka 1924.

Ajabu: Mchezaji ampiga refa kadi nyekundu, angalia hapa video
Uingereza yamwagia sifa Magufuli, yaahidi haya