Marais wanane wa nchi za Afrika wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru,yatayofanyika kesho katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Viongozi hao ni pamoja na Robert Mugabe (Zimbabwe), Joseph Kabila (DRC), Yoweri Museveni (Uganda), Piere Nkurunzinza (Burundi), Paul Kagame (Rwanda), Edger Lungu (Zambia), Uhuru Kenyatta (Kenya) na Denis Sassou Nguesso (Congo Brazaville).

Mkuu wa maandalizi ya gwaride, Brigedia Jenerali Dominiki Mrope  amesema sherehe za mwaka huu zitakuwa za kipekee na kila kitu kimekamilika.

“Gwaride limeandaliwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi, JKT, Polisi na Magereza, askali wote wana ari ya kuonyesha gwaride safi kesho, ikiwa ni mara ya kwanza tangu Rais John Magufuli aingie madarakani”amesema Jenerali Mrope.

Rais Magufuli alifuta sherehe za mwaka jana na kuifanya siku hiyo kuwa ya usfi nchi nzima.

Ahukumiwa miaka 3 kwa makosa ya mtandao
Maombi ya dhamana ya Lema kusikilizwa leo