Watu watatu akiwamo mtoto wa mwaka mmoja wamefariki dunia mkoani Tabora baada ya mvua iliyoambatana na radi kuunguza nyumba waliokuwemo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 25, 2021 katika kitongoji cha Mkuyuni, Kijiji cha Lumbulasiasa kata ya Ugunga Wilaya ya Kaliua.

Akizungumzia tukia hilo Kamanda Abwao amesema wakati mvua inanyesha, radi radi ilipiga na kuiunguza nyumba ambayo walikuwemo.

Waliofariki kuwa ni John Matelemki (48), Mbisi Maziku (28) na mtoto wa mwaka mmoja, Raphael John huku akitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua ambazo zimeanza kunyesha katika baadhi ya ya mkoa huo.

Ulega asisitiza uzalishaji bora wa nyavu
Uganda kupoteza uwanja wa Ndege wa kimataifa Entebe