Jeshi la Ulinzi la Kenya kwa kushirikiana na vikosi vya jeshi la Somalia wamefanikiwa kumkomboa mwalimu aliyekuwa ametekwa na kundi la Al Shabaab, Jumatatu wiki hii kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Dadaad, Garissa, Kenya.

Mwalimu huyo wa kike aliyetajwa kwa jina la Bi. Judy Mutui alikuwa mikononi mwa watekaji hao katika eneo la Shaba-Difu, Somalia, kilometa 15 kutoka Kenya ambapo mtekaji mmoja aliuawa na mwingine alikamatwa.

Jeshi la Kenya limeeleza kuwa mwalimu huyo anaendelea kupata matibabu na ataresafirishwa kwa ndege hadi jijini Nairobi baadaye.

Diamond Kushindana Na Mrembo Wa Dunia Toka India, Priyanka Chopra
Tanzia: Deo Filikunjombe, Capt. W Silaa Wafariki Kwa ajali Ya Chopa