Jopo la Majaji limetoa maamuzi juu ya kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabili mwanamke wa California aliyemuua mwanae aliyekuwa na umri wa mwezi mmoja kwa kumuoka kwenye ‘Oven’ mwaka 2011.

Jopo hilo limeukataa utetezi uliotolewa na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 aliyetajwa kwa jina la Ka Yang kuwa alikuwa na ugonjwa wa kifafa hivyo hakuwa anatambua alichokifanya wakati huo.

Jopo hilo la majaji limemkuta na hatia mwanamke huyo na hivi sasa anakabiriwa na kifungo cha miaka 26 jela ambacho atahukumiwa rasmi December mwaka huu.

Muendesha mashtaka alieleza kuwa mwanamke huyo alitumia kati ya dakika 2 na nusu na dakika 5 kumuoka mwanae huyo nyumbani kwake.

Mwanamke huyo ameolewa na ana watoto watatu.

 

Mwenyekiti wa Chadema Geita Auawa Kikatili
Islamic State latangaza kuhusika na shambulizi la Kigaidi Ufaransa