Mwanamuziki nguli wa Marekani, Prince Rogers Nelson maarufu kama ‘Prince’ aliyetikisa dunia ya muziki hususan miaka ya 1980 alipotamba na nyimbo kama Kiss na Purple Rain, amefariki jana katika jimbo la Minnesota.

Afisa Mwandamizi wa Jeshi Polisi la Minnesota, Jim Olson limeeleza kuwa Prince alikutwa akiwa hajitambui katika lifti iliyokoPaisley Park Studio jimboni humo, ndipo walipoamua kumkimbiza hospitali.

Olson ameeleza kuwa madaktari walijaribu kumfanyia tiba ya kumshtua moyo wake lakini hawakufanikiwa baada ya kubaini amefariki majira ya saa 4:07 asubuhi.

Mamlaka za Minnesota zimeeleza kuwa zinafanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake na kwamba zoezi la kumfanyia upasuaji kumchunguza litafanyika leo.

Ripoti iliyotolewa na TMZ, imeeleza kuwa chanzo cha kifo chake ni matumizi ya dawa za kulevya yaliyomzidi, siku sita kabla ya kifo chake.

Prince ni mwanamuziki mwenye heshima kubwa ambaye aliwahi kuleta upinzani kwa Marehemu, Mfalme wa Pop Dunian, Michael Jackson.

Lowassa azua tafrani Bungeni, apelekea Bunge kuahirishwa kwa muda
Magufuli kuwatumbua wanaowatetea 'aliowatumbua hadharani'