Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake hii leo Oktoba 6, 2022 Mkoani Kagera, ambapo unatarajia kukagua, kutembelea na kuzindua jumla ya miradi 37 ya Afya, Elimu, Maji, Barabara na miradi ya watu binafsi yenye thamani ya Tsh. bilioni 13.6, kwa Halmashauri nane za Mkoa huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022, Sahili Geraruma akiwa katika siku ya kwanza ya ukimbizaji wa Mwenge huo, amezindua mradi wa maji Ruganzu, uliopo Kata ya Nyanza, Wilaya ya Biharamulo wenye thamani ya Tsh. milion 114.3 uliojengwa na Shirika la Community Based Health Care Council (CBHCC), na nguvu za jamii.
Akiwa katika uzinduzi huo, amewasihi wananchi kuunganisha huduma ya maji katika makazi yao, ili kukamilisha dhana ya kumtua mama ndoo kichwani mara baada ya mradi wa maji wa Ruganzu kukamilika, ambapo kwa Wilaya ya Biharamulo, Mwenge huo umezindua mradi wa Maji Ruganzu na vyumba 2 vya madarasa Shule ya Wasichana Kagongo kwa fedha za Uviko-19.
Amesema, “Ili kuunga juhudi za Rais Samia za kumtua mama ndoo kichwani, yatupasa kuunganisha huduma ya Maji katika nyumba zetu, lakini kumuacha mama aendelee kufuata maji mita mia mbili au mita mia tatu tunakuwa bado hatujatimiza lengo hivyo nawasihi wananchi tuhakikishe kila mmoja wetu anaunganisha huduma ya maji.”
Katika Mkoa huo, miradi miwili ya barabara ya Lami ya Rukaragata-Kibamba km 1 na kituo cha Afya cha Bisibo imewekewa jiwe la msingi na pia kufanya ukaguzi wa shughuli za Lishe, mapambano dhidi ya Malaria, madawa ya kulevya na kuzindua klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Nyakanazi.
Aidha, amewashukuru wahisani CBHCC, kwa kutekeleza mradi huo kwa viwango na kuwasihi maeneo yote yaliyojengwa vituo vya kuchotea maji yawekewe uzio ili kuzuia hujuma kwenye miundombinu na kuwataka watalaam wanaosimamia miradi ya Serikali kuhakikisha wanafuata taratibu na maelekezo ya matumizi ya fedha kama.