Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa (BAVICHA) Patrobas Katambi ameomba ridhaa ya kujiunga na ChamaCha Mapinduzi CCM, leo kwenye kikao cha Halmashauri ya Kamati Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwa madai kwamba siyo kwa sababu ya madaraka bali kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Katambi amesema kuwa yupo tayari kuitwa msaliti kwa kusaliti ubinafsi na kundi la mabinafsi kwa ajili ya maslahi ya taifa.
“Naomba ridhaa ya kuwa mwanachama siyo kwa sababu ya madaraka bali kwa ajili ya maslahi ya taifa pamoja na kusaidiana na wenzangu kukiendeleza chama. Natambua harakati zilizofanyika kwenye awamu iliyopita. Watu wengi wanapenda lakini Hatupendi kubadilika na Mabadiliko yabnapoanza misuguano ndipo inapoanzia,”amesema Katambi
Hata hivyo, Katambi amesema kuwa ameona CCM inawapatia vijana nafasi na fursa za kuongoza tofauti na alipotoka kwamba vijana wakishatumiwa wanaonekana kama takataka yaani ni kama karai baada ya ujenzi.