Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Samson Mwigamba ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) mara baada ya siku za hivi karibuni kuachia ngazi ya uongozi na kuwa mwanachama wa kawaida wa chama hicho.
Mwigamba ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi habari ambapo amesema kuwa uamuzi wake huo unatokana na chama cha mapinduzi CCM kutimiza baadhi sera za ACT- Wazalendo.
Amesema kuwa CCM kimekuwa chama safi baada ya baadhi ya mafisadi kushughulikiwa na kukimbilia upinzani na upinzani kukosa sifa za walizokuwa nazo hivyo kukifanya CCM kuwa chama safi.
“Nimeamua kuhamia CCM kwa sababu siku hizi wamekuwa wakitimiza Ilani ya ACT- Wazalendo hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwa kwenye hicho chama, hivyo natoka ACT- Wazalendo bila ugomvi na mtu,”amesema Mwigamba
-
Nyumba yamtia matatani Zitto Kabwe
-
Lissu ampa ujumbe mzito Zitto, ‘Tumeshinda’
-
UVCCM: Rushwa bado ni tatizo kubwa
Hata hivyo, ameongeza kuwa chama cha ACT- Wazalendo kwa sasa wamejaa wanaharakati na wafuasi wa watu binafsi na si wafuasi wa chama husika kwakuwa misingi ya chama imekuwa ikikiukwa.