Mwimbaji wa bendi maarufu ya muziki wa rock  ya Linking Park, Chester Bennington amekutwa akiwa amekufa akisadikika kuwa amejiua.

Jeshi la polisi limeeleza kuwa lilifika nyumbani kwa mwimbaji huyo majira ya saa tatu asubuhi baada ya kupigiwa simu na kwamba kutokana na mazingira halisi waliyoyakuta wanaamini mwimbaji huyo alijiua.

Bennington aliyepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 41, alipata mafanikio makubwa zaidi kwenye muziki katika miaka ya 2000 akiwa na bendi yake ambayo iliachia albamu ya ‘Hybrid Theory’ iliyopata mafanikio makubwa.

Sauti yake ya pekee ndani ya bendi hiyo ilimfanya aonekane zaidi kama mwimbaji kiongozi aliyependwa na mashabiki wengi.

Mwimbaji huyo aliwahi kuliambia gazeti la The Guardian la Marekani kuwa amepitia maisha magumu yaliyosababisha kuwa teja wa dawa za kulevya. Alisimulia kuwa alipokuwa na umri wa miaka 11 wazazi wake walitalakiana na ndipo maisha yake yalipoanza kuwa magumu zaidi.

Bennington aliliambia the Guardian kuwa alifanyiwa ukatili na kubakwa mara kadhaa akiwa katika umri mdogo, hali ambayo ilivuruga akili yake na ikampa ukichaa unaoitesa saikolojia yake.

Watu wengi maarufu wameonesha kuguswa na kifo cha mwimbaji huyo, wakionesha hisia zao kupitia mitandao ya kijamii.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 21, 2017
Video: ADC wamnanga Lissu, wasema hana uzalendo