Chama cha Alliance for Democratic Change, (ADC) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) kuomba msamaha kufuatia matamshi ya Mwanasheria wake Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu aliyoyatoa siku za hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan Doyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  mapema hii leo jijiini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa matamshi hayo hayavumiliki kwa Mtanzania yeyote kusikia mwanasiasa mmoja akitaka kwenda kuishtaki nchi umoja wa mataifa ili isipate misaada.

Amesema kuwa kama Chadema wameshindwa kushindana kisiasa ni bora wakawaeleza wafuasi wao kuwa hawawezi kushindana na Chama Cha Mapinduzi CCM lakini si kuanza kuichongea nchi kimataifa.

“Hii ni nchi yetu sote, kamwe ugomvi wa ndani huwezi ukaupeleka nje hata siku moja, kwa hili wanalotaka kulifanya Chadema si jambo la kizalendo hata kidogo, wanataka kutuharibia nchi yetu, kama wameshindwa ni bora wakae pembeni,” amesema Doyo.

Mwimbaji maarufu Chester Bennington ajiua
Tundu Lissu akamatwa uwanja wa Ndege wa JNIA