Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi amemuomba kiongozi wa dini ya Wahindu ya Swaminarayan Duniani, Mahant Swami Maharaji kuiombea Tanzania amani na umoja viweze kudumu na kusiwepo aina yoyote ya ubaguzi kwa sasa na hata vizazi vijavyo.
Amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kumkaribisha kiongozi huyo hapa nchini na kukutana na waumini wa dini hiyo.
Aidha, Mwinyi ameshukuru kualikwa katika hafla hiyo ya kidini kwani sio jambo la kawaida kupokea ugeni wa kiongozi wa kidini nchini.
“Sina shaka kuwa sio nchi zote wenye kuwa na uwezo wa kumuona kiongozi mwenye nafasi kubwa kama hiyo katika nchi zote lakini Watanzania wamekuwa na bahati ya kumuona,” amesema Mwinyi.
Pia Mwinyi amemtaka kiongozi huyo kuiombea sana Tanzania ili iendelee kudumisha amani na umoja licha ya kutokuwepo kwa aina yoyote ya ubaguzi, wananchi waendelee kuishi kama ndugu.
Kwa upande wake, kiongozi huyo ambaye ni wa sita kwa nafasi hiyo, Maharaji amesema ataendelea kuiombea Tanzania na dunia nzima kwa ujumla ili wananchi wake waendelee kubarikiwa katika maisha yao pamoja na kukuza maendeleo yao.

Video: Itakuwa mshike mshike Bungeni, Lissu: Nilinusurika kupigwa na Wassira
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 2, 2017