Pamoja na Kikosi chake kuwa katika nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kikiwa na alama 22, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera, anapiga hesabu ya kuzichukua alama tisa ili kujiweka mahali salama.

Zahera amesema anahitaji kushinda katika mechi zote tatu zilizosalia ili kuendelea kubaki katika ligi hiyo na wataanza kwa kuiduwaza Mtibwa Sugar keshokutwa Jumatatu (Mei 15).

Kocha huyo wa zamani wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans amesema, bado anaimani na timu yake itafanya vizuri na kuwaondoa wasiwasi mashabiki wao hawatashuka daraja.

“Bado tunaimani ya kufanya vizuri katika hizi mechi tatu zilizosalia kwa kuhakikisha tunavuna pointi tisa zitakazotuondoa hapa chini, tukifanikiwa kupata hizo tutakuwa na alama 31 ambazo ni salama,” amesema kocha huyo kutoka DR Congo.

Ameongeza maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar yamekamilika na wataingia kwa tahadhari kwa sababu ndio michezo yao ya fainali iliyobakia.

Meridianbet Yaibukia Mbagala Kugawa Reflectors kwa Bodaboda
Odinga, Ruto uso kwa uso mazishi ya mpigania uhuru