Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekeko maarufu kama Mzee wa Upako amempiga tafu mkali wa Bongo Fleva, Q-Chillah katika wimbo wake mpya alioubatiza jina la ‘Naogopa’.
Chillah ambaye aliwahi kukiri kuwa alikuwa muathirika wa matumizi ya dawa za kulevya, alifunguka kupitia kipindi cha Nipe Tano cha TBC FM mwishoni mwa wiki iliyopita akieleza kuwa Mzee wa Upako alimpa kiasi cha fedha kugharamia kurekodi na kusambaza wimbo huo.
Muimbaji huyo amesema Mchungaji Lusekelo ni shabiki mkubwa wa kazi zake na kwamba amekuwa akimualika nyumbani kwake mara kadhaa.
“Kuna siku alinipigia simu ‘from nowhere’ na kuniambia napenda sana kazi zako,” alisema Q Chilla. “Na baada ya hapo nimekuwa nakutana naye mara nyingi na kupata nae dinner (chakula cha usiku) hata nyumbani kwake,” aliongeza.
- Video: Fid Q apigia mstari albam yake mpya, atoa siri ya kuachia mbili kwa mpigo
- Raila atangaza kutoa ‘neno zito’, Jeshi la Polisi lanena kuhusu tuhuma za mauaji
Hata hivyo, Q Chilla hakuwa tayari kuweka wazi kiwango cha fedha alichopewa na Mchungaji Lusekelo kuiwezesha ‘Naogopa’ kuingia sokoni.
‘Naogopa’ ambayo ilitambulishwa siku kadhaa zilizopita imeshaonesha kukubalika na mashabiki wengi nchini ndani ya muda mfupi.
Mbali na Q Chillah, Mzee wa Upako amewahi kuonesha mapenzi ya dhati kwa wimbo wa Darassa ‘Muziki’, ambao alitumia hata baadhi ya mashairi yake akiwa madhabahuni.