Meneja wa Man City Pep Guardiola ameonyesha matumaini ya kumtumia kiungo mshambuliaji wake kutoka nchini Ubelgiji Kevin de Bruyne, wakati wa mchezo wa mzunguuko wa tatu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona.

Guardiola amethibitisha kuwa na uhakika huo, alipozungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa mzunguuko wa pili hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Celtic ambao watakua nyumbani Celtic Park usiku wa leo.

De Bruyne alipatwa na maumivu ya nyonga mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa ligi ya nchini Uingereza dhidi ya Swansea City ambao walikubali kufungwa mabao matatu kwa moja.

Guardiola amesema taarifa za kitabibu zinaeleza kuwa De Bruyne anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma manne, lakini kwa maendeleo yaliopo hivi sasa kuna uwezekano wa kiungo huyo kujumuika na wenzake katika mchezo wa Oktoba 19.

De Bruyne amekua sehemu ya kikosi cha Man City ambacho kimefanikiwa kupata ushindi katika michezo sita iliyopita, jambo ambalo linahisiwa kukosekana kwake huenda kukaleta changamoto na kumpelekea Guardiola kutumia mbinu mbadala.

Guardiola pia anatarajia beki wa kati Vincent Kompany, ambaye alitonesha maumivu wa nyonga wakati wa mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Swansea City, atarejea tena uwanjani ndani ya majuma matatu yajayo.

Mwalimu amtia mimba mtoto wa darasa la 4, atuhumiwa kifungo cha miaka 32
Katibu Tawala, Muhasibu Mkuu na Mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba ni majipu