Zikiwa zimebaiki takribani siku 20 watanzania wamalize kile kinachoitwa zoezi la kumleta atakayeleta mabadiliko ya kweli, imeelezwa kuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho kitakachoibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, alipokuwa nchini Kenya na Rais Uhuru Kenyatta kwa ajili ya uzinduzi wa barabara muhimu ya Kilometa 98.4, ya Traveta-Voi-Mwatete, iliyofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB).

“Rais Kenyatta amenialika katika muda muafaka. Siku 21 tangu leo (jana) tutapiga kura kumchagua rais… Mnaniuliza nani? Atatoka kwenye chama changu. Sina shaka kuhusu hilo. Hii ni fursa nzuri kwangu kuwa hapa na kuwaaga wakenya,” alisema rais Kikwete.

Naye mwenyeji wake, Rais uhuru Kenyatta, ingawa hakutaja jina la chama, alieleza kuwa anaimani kuwa watanzania wataendelea kuisapoti serikali ambayo imewaletea amani kwa miaka yote.

Hata hivyo, kutokana na ushindani mkali uliopo ambao haujawahi kutokea katika historia ya uchaguzi mkuu nchini, kila chama kinajinadi kuwa na uhakika wa kushinda kwa kishindo.

CCM wanaamini mgombea wao Dk. John Magufuli atashinda, huku Chadema wanaamini kuwa mgombea wake, Edward Lowassa anaeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, atashinda uchaguzi mkuu huo bila shaka yoyote.

Kauli ya hiyo ya rais Kikwete ilikuja masaa machache kabla ya kutolewa taarifa rasmi za kuwateua wakuu wapya wa wilaya pamoja na kuwabadilisha vituo vya kazi baadhi ya wakuu wa wilaya ambapo majina 13 yalitajwa kwenye orodha hiyo.

Bale Atawala Kwa Ubora Nchini Wales
Rodgers Apewa Nafasi Nyingine Ligi Ya England