Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema anatarajia kumuona tena aliyekua meneja wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers akirejea kwenye medani ya ufundishaji wa soka wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Wenger, alisisitiza kusikitishwa na hatua ya kutimuliwa kwa meneja huyo kutoka Ireland ya kaskazini, kwa kusema haukua muda sahihi kwa viongozi wa Liverpool kuchukua maamuzi mazito ya kuachana na Rodgers.

Amesema Rodgers ni meneja mwenye vigezo vyote vya kuwa na klabu kubwa kama Liverpool, na viongozi wa The Reds walipaswa kumuacha kwa kuangalia matarajio ya baadae ya klabu hiyo ambayo ilionyesha kubadili mfumo.

Hata hivyo Wenger amesema kutokana na ubora wa meneja huyo, amekiri kutokua na shaka ya kumuona akirejea tena katika benchi la ufundi la moja ya klabu za nchini England na kufanya vyema.

Rodgers, alitimuliwa kazi mara baada ya mchezo wa ligi ya nchini England, kati ya Liverpool na Everton ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

‘Na Uhakika, CCM Itashinda Uchaguzi Mkuu’
Kibopa Wa Mbeya City Atoa Tamko Dhidi Ya Nyosso