Kocha Mkuu wa Young Africans, Nabi Nasreddine amesema alikutana na Simba SC kwa mara ya kwanza msimu huu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati huo anafundisha El Marreikh ya Sudan.

Nabi amesema kuna baadhi ya vitu ambavyo alitumia katika mchezo ule uliochezwa Sudan na kumalizika kwa suluhu atavifanya tena katika mchezo wa kesho Jumamosi (Julai 03), na akasisitiza kwamba hazungumzi sana wao watatenda kufanya vitendo kwenye Uwanja wa Mkapa.

“Kama ambavyo wao wanatamani kushinda, basi nasi ni hivyohivyo, tusubiri muda wa mechi ufike tuone namna gani ushindani ambao tutautoa na kupata kile ambacho tunahitaji,” amesema Nabi ambaye amekiri kusikia tambo za Simba SC kwamba watashinda mchezo huo.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Tunisia na Ubelgiji, alipocheza mara ya kwanza na Simba SC iliyokuwa chini ya kocha Didier Gomes, licha ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu jijini Khartoum huko Sudan muda mfupi baadaye alifukuzwa kazi na miezi kadhaa baadae alijiunga na Young Africans.

Kwa mara ya kwanza kesho Jumamosi (Julai 03) Kocha Nabi atakiongoza kikosi cha Young Africans kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC.

vibaka, majambazi watafute kazi nyingine - Kamanda Kyando
Rage: Mchakato uchaguzi TFF uko sawa