Chama cha soka nchini Tunisia kimemteua kocha mzawa, Nabil Maaloul kuwa mkuu mpya wa benchi la ufundi la timu ya taifa hilo maarufu kwa jina la ‘Eagles of Carthage’.

Maaloul ambaye aliwahi kuwa kocha wa klabu za Espérance Sportive de Tunis (Tunisia) na El-Jaish SC (Qatar) anachukua mikoba ya Mpoland, Henryk Kasperczak aliyefutwa kazi mapema mwaka huu.

Kasperczak alifutwa kazi baada ya Tunisia kushindwa kutamba kwenye fainali zilizopita za michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon na Cameroon kuibuka mabingwa.

Maaloul mwenye umri wa miaka 54, anarejea kuifundisha Tunisia kwa mara ya pili. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2013 ambapo alihudumu kwa miezi saba pekee kabla ya kutimkia nchini Kuwait ambapo alipewa kibarua cha kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo.

Jukumu kubwa linalomkabili Maaloul ni kuhakikisha Tunisia inafuzu michuano ya AFCON ya mwaka 2019 ambapo imepanga kundi J pamoja na mataifa ya Misri, Niger na Swaziland.

Video: Coyo MC na Maajabu Aliyoyaona Jukwaani, awataja Fid Q na Young Killer
Lowassa Aahidi Kumpigia Kampeni Kenyatta Uchaguzi Kenya