Beki wa kushoto wa Arsenal, Nacho Monreal amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo ya London. Monreal, 29, alijunga na Arsenal mwezi Januari 2013 akitokea Malaga ya Spain.

Beki huyo amecheza mechi 113, zikiwemo mechi zote 22 za ligi kuu msimu huu. “Nilikutana na boss (Arsene Wenger) miaka mitatu iliyopita na tumekuwa na uhusiano mzuri na nina furahia kuwepo hapa.

Kwa sababu hizo nimeongeza mkataba wangu,” amesema.

Wenger amesema: “Ni mchezaji muhimu sana katika klabu, kwa sababu anaweza kucheza kushoto na kati. Kiwango chake cha uchezaji kimekuwa cha juu muda wote na hilo linahitajika katika ngazi kama hii.”
Muda hasa wa mkataba huo haujatajwa.

Israel yamwagia sifa Rais Magufuli, yaahidi ushirikiano
Zari na Wema Sepetu wapeana 'Makavu' kwenye mtandao