Fununua za kuwa msanii Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii wenye maringo na kuwa na tabia ya majivuno hasa kutopenda maendeleo ya wasanii wengine zimemuibua mwanamuziki Mtanzania anayeishi nchini Marekani Mr Lambert, ambaye ametoa ya kwake ya moyoni kuhusu uvumi huo kwa kuwaeleza alichokiona baada ya kukutana uso kwa uso na msanii Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Mr Lambert ameandika “acha niwe muwazi hasa kwa wale watu wenye tabia za kuwasemea watu uongo, several times nimesikia watu wakisema Diamond Platnums hapendi wasanii wengine na anapenda kuwa juu yeye tu, jambo ambalo nadhani kuna watu wanakubaliana na hilo swala sababu labda hawajawahi kupata nafasi ya kujua ukweli.

Kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kukutana na Diamond Platnums na kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kushiriki jukwaa moja na yeye.

Lakini kitu kimoja ambacho nitaheshimu milele ni furaha yake kujua kwamba kuna wasanii Kama sisi ambao tunaishi nchini Marekani lakini bado tunapambana kukuza kiswahili na kufanya muziki tukiwa huku huku.

Hanijui Ila Diamond nikiri kusema alitumia muda wake ambao angefanya mambo mengine ila aliniweka chini na kunishauri mambo mengi sana juu ya Sanaa lakini kubwa zaidi ni kuniambia tuendelee kupambana kuhakikisha Swahili Nation inafika Duniani kote.

Nashangaa msanii kama Diamond Platnumz ambaye hatujawahi kutana ila ametumia muda wake kunishauri mambo makubwa kwa faida yangu maneno ya kwamba anaringa sijui anapenda wengine washuke yanatoka wapi.

My brother once again thanks so much can’t wait kukutana na wewe next time nikija Tanzania na nakuombea watu wazidi kujua thamani na upendo wako kwa watu wengine.

If you don’t have any nice word to say to someone so don’t force bad to came to you so you can have something to say. Much respect Diamond Plantumz”. Aliandika Mr Lambert.

Pamoja na hayo msanii Diamond platnumz amemaliza ziara yake ya kikazi nchini Marekani alikokwenda kwaajili ya kutumbuiza kwenye Matamasha kadhaa, hivyo kwa sasa yuko mbioni kurejea nchini kuendelea na majukumu yake mengine ikiwa ni pamoja na maandalizi ya album yake mpya inayotarajiwa kuingia sokoni mapema mwisho wa mwaka huu.

Antonio Conte aahidiwa mabilioni ya shilingi
TFF yakemea vurugu viwanjani