Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa ubunifu wanaouonyesha katika kuelezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano.
Ameyasema hayo siku moja baada ya kumwagiza Mkurugenzi wa Habari Maelezo, kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kuona kama utendaji wao unaleta tija kwa jamii.
Aidha, Nape amesema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili maafisa mawasiliano wa Serikali, kurugenzi za mawasiliano Ikulu na Idara ya habari maelezo wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali.
 “Nawapongeza wakurugenzi vijana, Dkt. Hassan Abbasi (Maelezo) na Greyson Msigwa wa Ikulu.  Hawa ni mfano wa ubunifu  wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa,”amesema Nape.
Hata hivyo, Nape amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini.

Yanga Kuifuata Zanaco Bila Ngoma, Tambwe
Magazeti ya Tanzania leo Machi 16, 2017