Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameitaka timu ya soka ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars kususia mechi na Libya, kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea Libya.
Ameyasema hayo, katika ukurasa wake wa twitter, ambapo amesema kuwa ni vyema timu ya Kilimanjaro Stars ikasusia mchezo huo.
“Nashauri Tanzania isiingie uwanjani kucheza na Libya. SADC iagize nchi zake zote zirudishe mabalozi wake kutoka Libya, ili kuonyesha kuchukizwa na Biashara ya Utumwa,”ameandika Zitto
Aidha, Zitto amewataka Watanzania wachukue hatua kuonyesha kuchukizwa na kupinga vitendo hivyo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu, vinavyoendelea nchini Libya.
-
Ujenzi wa machinjio ya kisasa ukamilike kabla ya Desemba- Mpina
-
Tanesco yawaomba radhi wateja wake
-
Tanzania na Ujerumani zatenga bilioni 375.4
- Hata hivyo, hivi karibuni kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Libya baada ya kuibuka biashara ya utumwa, huku mataifa mbali mbali ya Afrika yakikaa kimya bila kutoa maamuzi dhidi ya vitendo hivyo vyenye historia mbaya.