Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewaomba radhi wateja wake waliopo katika mikoa yote iliyounganishwa katika Gridi ya taifa mara baada ya kujitokeza hitilafu iliyosababisha kukatika kwa umeme.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo mapema hii leo imesema kuwa tatizo hilo linashughulikiwa hivyo wananchi wanatakiwa kuwa watulivu wakati jitihada za kurejesha umeme zikifanyika.

Hata hivyo, taarifa hiyo imewataka wananchi kutokusogelea wala kugusa nyaya ziliokatika na kudondoka hivyo watoe taarifa.

Video: Lissu asimulia mambo mazito kwa dakika 60, Mchezo mchafu tena bandarini
Tanzania na Ujerumani zatenga bilioni 375.4