Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi wa Watumishi Housing Dkt. Fred Msemwa kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa nyumba 35 za walimu ambazo kampuni hiyo imetakiwa kuzijenga.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo hii  leo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Nyumba za walimu na ujenzi wa shule za Sekondari  zilizopo kwenye wilaya ya Ilala  ambapo tayari Wizara imetoa kiasi cha shilingi  5.6  kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba hizo.

Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako ametembelea na kukagua shule ya Sekondari  Msongola, Nyumba za walimu,  shule ya Sekondari Mvuti na shule kongwe ya Sekondari Pugu zote zilizopo katika manispaa ya Ilala, mkoani Dar es salaam.

Kingue aongozewa mwaka mmoja Azam FC
Video: Mnangagwa aapishwa kuwa Rais Zimbabwe