Picha za zinazoonesha Wema Sepetu na raia wa Namibia Luis Munana aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Hot Shots zimepata maelezo kutoka kwa mhusika.

Baada ya wiki moja ya sintofahamu ya picha hizo zilizokosa maelezo kama kilichooneshwa ni uhalisia au ni picha zilizopigwa kwenye scene ya filamu ijayo, Luis amethibitisha kuwa picha hizo ni za tukio halisi lililoshuhudiwa na wazazi wa pande zote mbili.

Ingawa hakueleza kwa undani kilichofanyika kwa madai ya kuwa ilikuwa faragha, Luis alikiri kuwa yeye na Wema walijikuta wamezama kwenye kina cha mapenzi katika siku yao ya kwanza tu kuonana kwenye Instagram Party.

“Alikuwa crush wangu, nami nilikuwa crush wake,” Luis aliiambia Clouds TV.

 

 

Walichoamua Ukawa Kuhusu Kuapishwa Dkt. Magufuli
Hiki Ndicho Rais Kagame Amemuandikia Rais Mteule Dkt. Magufuli