Eva Godwin – Dodoma.

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali – NGO’s, yanayojihusisha na masuala ya Mazingira kukutana na kufanya tathmini juu ya utunzaji wa Mazingira unavyotekelezwa Jijini Dodoma, kwa kila robo ya Mwaka wa Fedha.

Gugu ameyasema hayo hii leo Oktoba 23, 2023 katika kikao kazi cha Utunzaji wa Mazingira kwa mashirika hayo yaliyopo Mkoani Dodoma,amesema wanaona juhudi za Serikali ya awamu ya sita ipo karibu sana na Taasisi ambazo ziko nje ya Serikali na mchango wao unaonekana zaidi katika kuyalinda Mazingira.

“Tunaona mchango mkubwa ambao unafanywa na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Mhe.Samia Suluhu,mpo karibu na taasisi zisizo za kiserikali katika kuhakikisha tunaenda sawa ma taasisi za kiserikali katika kuyalinda mazingira,”amesema.

Aidha, ameongeza kuwa mkutano huo ni fursa ya kutambuana na kujua shughuli zinazofanywa na kila mmoja na kwamba watakapokutana kwa kila robo ya Mwaka wa Fedha watajadiliana na kufanya tathmini ya kazi zinazofanyika.

Kikao kazi hicho, kimeyajumusisha mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na Utunzaji na Usafi wa mazingira kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma, huku lengo kuu likiwa ni kujadili na kuweka mikakati inayohusiana na Mazingira, hususani katika Makao makuu ya Nchi.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 24, 2023
Chemba kufuatilia, kuimarisha vyanzo vya mapato